Azam, Yanga na Simba zachuana vikali Ligi ya Tanzania

media

Timu za Azam, Simba na Yanga zinaendelea kuchuana vikali katika ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Azam baada ya kucheza mechi 11 imefikisha alama 27, jana iliishinda Singida United ya Singida kwa bao 1-0.
Simba ilifikisha alama 23 baada ya jana kuibandika Rivu Shootinga mabao 5-0 huku mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi akifunga mabao matatu katika mchezo huo na kufikisha jumla ya mabao saba aliyofunga msimu huu.
Hata hivyo Simba imecheza mechi 10, pungufu ya mchezo mmoja dhidi ya Azam.
Yanga ambao ni mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo watashuka uwanjani leo kuchuana na Lipuli ya Iringa wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliopita dhidi ya KMC.
Yanga ina alama 22 baada ya kushuka uwanjani mara nane na inaweza kuiengua Simba katika nafasi ya pili ikiwa itapata ushindi katika mchuano wa leo.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!