Barcelona bila Messi yailima Real Madrid 5-1



Klabu ya Barcelona imeibuka na ushindi mnono kwenye uwanja wake wa nyumbani baada ya kuishushia  Real Madrid kikapu cha mabao 4-1 kwenye mchezo wa La Liga.
Mabao ya Barcelona yaliwekwa wavuni na Philippe Coutinho (11’),  Luis Suares (dk 30,75,83) huku Arturo Vidal akiweka msumari wa mwisho dakika ya 87’ huku bao la Real Madrid liliwekwa wavuni na Marcelo Vieira.
Ushindi huo umeweka rehani kibarua cha kocha wao  ambaye hivi karibuni amekuwa akitajwa kuwa kwenye kikaango cha kutimuliwa muda wowote.
Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkali licha ya mashabiki wengi kufikiri kuwa kutokuwapo kwa Messi na Cristiano Ronaldo kama ilivyozoeleka, waliamini usingekuwa na radha.
Awali kabla ya mchezo, mshambuliaji mahiri wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann, alisema Barcelona itaichapa Real Madrid licha ya kukosekana kwa nahodha Lionel Messi aliyevunjika mkono.
Griezmann alisema sababu ya kuipa Barcelona nafasi ya kushinda mchezo huo ni rekodi yao nzuri kwenye Uwanja wake wa Nou Camp, kwani haijapoteza mechi yoyote kwa takribani miezi kumi pamoja na udhaifu wa Real imeonyesha katika ligi msimu huu.
Mshambuliaji huyo alisema Real iliyomkosa Cristiano Ronaldo aliyeondoka na kujiunga na Juventus, imepoteza ubora hususani katika safu yake ya ushambuliaji, hivyo hana shaka kuwa itapoteza mchezo huo.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!