Mmiliki wa Leicester City athibitishwa kufariki katika ajali ya Helikopta


media

Klabu ya Leicester City inaomboleza msiba wa mmiliki wake Vichai Srivaddhanaprabha ambaye amethibitishwa kuwa alipoteza maisha katika ajali ya helikopta iliyotokea mwishoni mwa juma.
Vichai Srivaddhanaprabha alikuwa sanjari na watu wengine wanne katika ndege hiyo ndogo ambayo ilianguka nje ya Uwanja wa king Power, punde  baada ya kushuhudia mchezo wa ligi Kuu mwishoni mwa Juma baina ya klabu yake na West Ham United.
Klabu yake imesema alikuwa mtu muhimu na aliyebadili fikra za mashabiki wa soka nchini Uingereza wakati alipoiongoza klabu hiyo kunyakua taji la Ligi Kuu mwaka 2016 mbele ya vigogo Chelsea, Manchester United na Liverpool.
Kifo cha Vichai Srivaddhanaprabha kimeibua hisia duniani kote ambapo mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa wakitoa salamu za rambirambi kwa kuweka mashada ya maua katika eneo ilipotokea ajali.
Aidha wachezaji mbalimbali wa soka na wastaafu akiwemo Didier Drogba, Wilfred Ndidi wamemiminika mitandao kutoa salamu za rambirambi kufuatia msiba huo.
Vichai Srivaddhanaprabha ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 60, licha ya alama aliyoweka kwenye mchezo wa soka anakumbukwa na raia wengi wa Thailand kwa mchango mkubwa aliotoa katika maendeleo ya taifa hilo.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!