Posts

Showing posts from October, 2018

Mmiliki wa Leicester City athibitishwa kufariki katika ajali ya Helikopta

Image
Klabu ya Leicester City inaomboleza msiba wa mmiliki wake Vichai Srivaddhanaprabha ambaye amethibitishwa kuwa alipoteza maisha katika ajali ya helikopta iliyotokea mwishoni mwa juma. Vichai Srivaddhanaprabha alikuwa sanjari na watu wengine wanne katika ndege hiyo ndogo ambayo ilianguka nje ya Uwanja wa king Power, punde  baada ya kushuhudia mchezo wa ligi Kuu mwishoni mwa Juma baina ya klabu yake na West Ham United. Klabu yake imesema alikuwa mtu muhimu na aliyebadili fikra za mashabiki wa soka nchini Uingereza wakati alipoiongoza klabu hiyo kunyakua taji la Ligi Kuu mwaka 2016 mbele ya vigogo Chelsea, Manchester United na Liverpool. Kifo cha Vichai Srivaddhanaprabha kimeibua hisia duniani kote ambapo mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa wakitoa salamu za rambirambi kwa kuweka mashada ya maua katika eneo ilipotokea ajali. Aidha wachezaji mbalimbali wa soka na wastaafu akiwemo Didier Drogba, Wilfred Ndidi wamemiminika mitandao kutoa salamu za rambirambi kufuatia msiba huo...

Azam, Yanga na Simba zachuana vikali Ligi ya Tanzania

Image
Timu za Azam, Simba na Yanga zinaendelea kuchuana vikali katika ligi Kuu ya Tanzania Bara. Azam baada ya kucheza mechi 11 imefikisha alama 27, jana iliishinda Singida United ya Singida kwa bao 1-0. Simba ilifikisha alama 23 baada ya jana kuibandika Rivu Shootinga mabao 5-0 huku mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi akifunga mabao matatu katika mchezo huo na kufikisha jumla ya mabao saba aliyofunga msimu huu. Hata hivyo Simba imecheza mechi 10, pungufu ya mchezo mmoja dhidi ya Azam. Yanga ambao ni mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo watashuka uwanjani leo kuchuana na Lipuli ya Iringa wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliopita dhidi ya KMC. Yanga ina alama 22 baada ya kushuka uwanjani mara nane na inaweza kuiengua Simba katika nafasi ya pili ikiwa itapata ushindi katika mchuano wa leo.

Barcelona bila Messi yailima Real Madrid 5-1

Image
Mabao ya Barcelona yaliwekwa wavuni na Philippe Coutinho (11’),  Luis Suares (dk 30,75,83) huku Arturo Vidal akiweka msumari wa mwisho dakika ya 87’ huku bao la Real Madrid liliwekwa wavuni na Marcelo Vieira. ADVERTISEMENT Klabu ya Barcelona imeibuka na ushindi mnono kwenye uwanja wake wa nyumbani baada ya kuishushia  Real Madrid kikapu cha mabao 4-1 kwenye mchezo wa La Liga. Mabao ya Barcelona yaliwekwa wavuni na Philippe Coutinho (11’),  Luis Suares (dk 30,75,83) huku Arturo Vidal akiweka msumari wa mwisho dakika ya 87’ huku bao la Real Madrid liliwekwa wavuni na Marcelo Vieira. Ushindi huo umeweka rehani kibarua cha kocha wao  ambaye hivi karibuni amekuwa akitajwa kuwa kwenye kikaango cha kutimuliwa muda wowote. Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkali licha ya mashabiki wengi kufikiri kuwa kutokuwapo kwa Messi na Cristiano Ronaldo kama ilivyozoeleka, waliamini usingekuwa na radha. Awali kabla ya mchezo, mshambuliaji mahiri wa Atletico Madr...

Okwi awafanyia mauaji Ruvu Shooting

Image
Mshambuliaji Emmanuel Okwi ameendeleza rekodi yake tamu dhidi ya Ruvu Shooting baada ya leo kufumania nyavu mara tatu 'hat tricks' katika ushindi wa mabao 5-0 ambao Simba wameupata kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Okwi alifunga mabao hayo katika dakika ya nane, dakika ya 53 na ile ya 77 katika mechi hiyo na kukaribia kurudia kile alichokifanya msimu uliopita alipowafunga Maafande hao mabao manne peke yake kwenye ushindi wa mabao 7-0 ambao Simba ilipata kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi. Katika mchezo huo uliotawaliwa zaidi na Simba, mabao mengine yalifungwa na Meddie Kagere na Adam Salamba. Washambuliaji Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na John Bocco leo walianza pamoja katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Simba ikiwa ni baada ya mechi tano kupita tangu walipoanzishwa hivyo. Wachgezaji hao watatu mara ya mwisho walianzishwa kwenye kikosi cha kwanza Septemba 15 kwenye mchezo wa ugenini dhidi ya Ndanda ambao ulimalizika kwa sa...

STRAIKA WA MIL 100 SIMBA MGUU NDANI, NJE

Image
D IRISHA  dogo la usajili linafunguliwa Novemba 15 mwaka huu, tayari mambo ni moto kwani ndani ya Simba, mshambuliaji wa timu hiyo, Mohammed Rashid huenda akaonyeshwa mlango wa kutokea. Rashid alisajiliwa na Simba msimu huu akitokea Prisons kwa dau la Sh mil 30 na mshahara wake unaonyesha analipwa Sh Mil 3 hivyo ukijumlisha kwa miaka miwili aliyosaini, jumla ataingiza Sh 102m. Simba imejaza washambuliaji wengi kwenye kikosi chao kiasi cha wengine kukosa nafasi ya kucheza mpaka sasa hivyo Rashid amekuwa akitajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji watakaoondolewa na atarudishwa Prisons kwa mkopo kwani kocha Patrick Aussems hajavutiwa na uwezo wake. Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba ambazo Championi Jumamosi limezipata zimedai kuwa, kuna uwezekano mkubwa klabu hiyo kutoongeza mchezaji yeyote kwenye dirisha dogo zaidi ya kuangalia wale ambao hawapati nafasi sana na kuwatoa kwa mkopo. “Ishu ya usajili katika dirisha dogo kuna uwezekano mkubwa wa kutoongeza mchezaji ...

CANNAVARO APEWA KUKU

Image
B EKI  na nahodha wa zamani wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, jana alifanyiwa ‘sapraiz’ ya kutosha kutoka kwa mashabiki wa Yanga kutoka Kijiji cha Chigungu kilichopo Masasi mkoani Mtwara. Mashabiki hao walikuwa barabarani kuusubiri msafara wa Cannavaro ambaye kwa sasa ni meneja wa Yanga uliokuwa unaenda Mtwara kufungua Tawi la Yanga. Msafara huo ukiwa njiani, ulisimamishwa na mashabiki hao ambapo wazee wa eneo hilo walimkabidhi Cannavaro katoni nne za maji huku wakimwambia akirudi apitie kuchukua kuku wake kama zawadi.

KITENGE WA STAND: JUUKO SIYO MTU MZURI

Image
STRAIKA wa Stand United, raia wa Burundi, Alex Kitenge amefunguka kuwa alishindwa kuwafunga Simba kwenye mchezo wao uliopigwa wiki iliyopita Uwanja wa Taifa na timu yake kupokea kichapo cha mabao 3-0, kutokana na uimara wa safu ya ulinzi ya Simba, huku akiweka wazi kuwa Juuko Murshid ni kiboko ya mabeki wote ambao amekutana nao msimu huu. Kitenge alishindwa kufurukuta tofauti na matarajio ya wengi ambapo mwanzoni mwa msimu alijiandikia historia ya kufunga mabao matatu ‘hat trick’ ya kwanza dhidi ya Yanga, licha ya timu yake kupoteza kwa mabao 4-3. Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa hali iliyozua mshituko kwa wapenda soka wengi na kuhisi kuwa jamaa atakuwa moto mkali katika kila mchezo. Akizungumza na  Championi Ijumaa,  Kitenge alisema mabeki wa Simba walimsumbua sana tofauti na alivyotarajia, huku akimtaja Mganda Juuko kuwa ni kiboko yao maana alikuwa anamfuata kila mahali ili asipate nafasi hata  ya kutuliza mpira, kitendo ambacho alifanikiwa na ...

MABAO YA OKWI, CHAMA YAMPONZA KICHUYA

Image
U SISHANGAE  kuona kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya akianzia benchi huku akiwapisha mastaa Mganda, Emmanuel Okwi na Mzambia, Claytous Chama wakicheza nafasi zake kutokana na ukame wa mabao alionao. Kichuya hadi hivi sasa amefunga bao moja pekee akiwa amecheza michezo nane tangu Ligi Kuu Bara imeanza, akianza katika kikosi cha kwanza tofauti na mchezo uliopita na Alliance FC ambao alikaa benchi. Wakati Kichuya akifunga bao moja, wenzake Meddie Kagere na Okwi wamefunga manne kila mmoja huku Chama akifunga mawili katika michezo miwili mfululizo pamoja na kuonyesha uwezo wa juu. Kichuya anatarajiwa kupata ugumu wa namba baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Patrick Aussems kufanya mabadiliko ya haraka katika kikosi chake kwa kuwahamisha Okwi na Chama kucheza viungo wanaotokea pembeni namba 7 na 11 nafasi inayochezwa na kiungo huyo. Akizungumza na  Championi Ijumaa,  Aussems alisema anataka kuwa na washambuliaji wenye uwezo wa kufunga mabao na ...