SIMBA SC YAIFANYIA UMAFIA YANGA SC
IMBA imeingia kwenye anga za Yanga, baada ya kocha Patrick Aussems kumfukuzia beki anayewaniwa na vinara hao wa Ligi Kuu Bara. Wekundu wa Msimbazi, juzi Jumamosi walitupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa 4-1 na TP Mazembe mjini Lubumbashi, na sasa hasira zao wanazihamishia kwenye Ligi Kuu Bara ili wapate nafasi nyingine ya kucheza Ligi ya Mabingwa mwakani. Tayari uongozi wa Simba umeshaanza mikakati ya kuwasaka wachezaji wakubwa ili wawe na nguvu zaidi msimu ujao wa Ligi ya Mabingwa, na wanataka wavuke hatua ya robo fainali ambayo wamekomea msimu huu. “Tumejifunza vitu vingi hadi hatua hii ambayo tumefikia na kutolewa. Tumeona kwamba ili usonge mbele kwenye hatua kubwa ni lazima uwe na wachezaji wenye viwango vikubwa na sisi kwa mwakani tutalifanyia kazi hilo,” alisema jana Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori. Kocha Patrick Aussems. Baada ya mechi hiyo ya ambayo ilichezwa huko Lubumbashi nchini DR Congo na Simba kufungwa mabao 4-1, kocha m...