SIMBA WASINGIZIA JAMHURI MOROGORO



KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, anakuna kichwa juu ya mbinu gani atumie wakati kikosi hicho kikiwa kinacheza katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro baada ya kusema wazi uwanja huo ni mbovu
na hauendani na staili wanayocheza.
Simba wamelazimika kuhamia huko baada ya Uwanja wa Taifa waliokuwa wanautumia kupigwa kufuli kwa ajili ya matengenezo kabla ya Afcon ya vijana.
“Ndiyo tunaweza kuathirika kwa namna fulani kwa sababu pale Taifa sehemu ya kuchezea ni safi tofauti na Morogoro ambapo tunaenda kucheza kwa sasa.

“Tunahama kutoka sehemu nzuri na kwenda pasipo pazuri. Pale sehemu yake ya kuchezea wala siyo rafiki sana, kucheza pale inabidi tujiandae sana bila ya hivyo inaweza kutukwamisha na kushindwa kupata ushindi,” alimaliza kocha huyo aliyejenga imani kwa mashabiki wa Simba.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!