Kocha Uganda amuita beki Dortmund kuivaa Taifa Stars

Kampala, Uganda. Kocha wa Uganda Cranes, Sebastien Desabre amemwita beki wa Borussia Dortmund, Herbert Bockhorn katika kikosi chake cha wachezaji 46, kinachojianda kwa mchezo wa mwisho wa Kundi L wa kusaka kufuzu AFCON 2019 dhidi Tanzania.
Katika orodha ya wachezaji 15, wanaocheza soka kulipwa nje beki wa kulia wa Dortmund, Bockhorn ameitwaa kwa mara kwanza katika kikosi hicho.
Mbali ya beki huyo pia kipa wa Adama City FC, Robert Odongkara, na beki wa Maroons, Brian Majwega wamerudishwa kikosini baada ya kuachwa kwa muda mrefu.
Kiungo anayechipukiza kwa sasa wa Mbarara City, Ivan Eyam ni miongoni mwa wachezaji 31 wanaocheza soka la ndani walioitwa kwa ajili ya kambi na baada ya mchujo watapatikana wachezaji tisa kuungana na wake 15 wa kulipwa na kuingia kambini Cairo.
Pia wapo winga Moses Opondo anayecheza VendsysselFF ya Denmark pamoja na Muhammed Shaban (Raja Casablanca, Morocco) ambao walikosa mechi zilizopita dhidi ya Tanzania na Lesotho.
Wachezaji 15 wa kulipwa na wale 9 kutoka ndani wataungana katika kambi Cairo, Misri kuanzia Machi 18 hadi 22, 2019.
Wachezaji wawili wazoefu Hassan Wasswa Mawanda na Godfrey Walusimbi wasiokuwa na timu kwa sasa wameitwaa katika kikosi cha wachezaji wa ndani wanaoendelea na mazoezi.
Kocha Desabre alisema tunataka kucheza mpira wetu na kuhakikisha tunapata matokeo mazuri dhidi ya Tanzania, ndiyo maana nimemwita kwa mara ya kwanza mchezaji kutoka Ujerumani katika kikosi changu.
“Ni matumaini yangu wataifanya kazi vizuri, nimeridhishwa na viwango vya wachezaji wa ndani. Katika kipindi cha kambi kwa wachezaji wa ndani nitawachagua tisa kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars. Pia, kambi hii ya wachezaji wa ndani itakuwa nafasi kwetu kujiandaa mapema kwa ajili ya mchezo wa kusaka kufuzu wa CHAN 2020, dhidi ya Sudan Kusini kati ya Julai na Agosti,” alisema kocha Desabre.
Nyota 15 wa kulipwa ni: Denis Onyango (Mamelodi Sundowns, Afrika Kusini), Jamal Salim (Al Hilah Omdruman, Sudan), Robert Odongkara ( Adama City FC, Ethiopia), Murushid Juuko (Simba, Tanzania), Denis Iguma ( Kazma, Kuwait), Nico Wakiro Wadada Azam FC, Tanzania), Herbert Bockhorn (Borussia Dortmund, Ujerumani), Moses Opondo (VendsysselFF, Denmark), Joseph Ochaya (TP Mazembe, DR Congo), Khalid Aucho (Church Hill Brothers, India), Faruku Miya (Gorica, Croatia), Edris Lubega (SV Reid, Austria), Emmanuel Okwi (Simba, Tanzania), Karisa Milton (MC Oujda, Morocco), Muhammad Shaban (Raja Casablanca, Morocco)
Wachezaji 31 wa ndani:
Nicholas Sebwato (Onduparaka Fc), Saidi Keni (Sc Villa), James Alitho (URA FC), Charles Lukwago (KCCA FC), Filbert Obenchan (KCCA FC), Paul Willa (Police FC), Samson Mutyaba (Maroons FC), Mustafa Kizza (KCCA FC), Majwega Brian (Maroons FC), Timothy Awanyi (KCCA FC), Paul Mbowa Baker (URA FC), Mujuzi Musitafa (Proline FC), Halid Lwaliwa (Vipers SC), Rashid Toha ( Onduparaka FC), Ibrahim Sadam Juma (KCCA FC), Ivan Eyam (Mbarara City FC), Taddeo Lwanga (Vipers SC), Okello Allan (KCCA FC), Waisswa Moses (Vipers SC), Bright Anukani (Proline FC), Owori David (Sc Villa), Allan Kyambadde (KCCA FC), Micheal Birungi (Express FC), Julius Poloto (KCCA), Juma Balinya (Police FC), Serunkuma Daniel (Vipers SC), Patrick Henry Kaddu (KCCA FC), Joel Madondo (Kirinya-Jinja SS), Bashir Mutanda (Sc Villa)
Pamoja na Godfrey Walusimbi na Hassan Wasswa Mawanda (hawana timu)
Comments
Post a Comment