SAFARI YA EDEN HAZARD KWENDA REAL MADRID IMEKOLEA
Mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard anasema: "Pengine ni wakati wa kujaribu mambo tofauti baada ya miaka 6 ya kuvutia Stamford Bridge.”
Kiungo huo mwenye miaka 27, aliyeihakikishia Ubelgiji ushindi dhidi ya Uingereza kwa kufunga bao la pili, waliposhinda 2-0 mechi ya kuwania nafasi ya tatu Kombe la Dunia, amehusishwa na kuhamia Real Madrid.
"Mnajua ni wapi natamani kutua," Hazard aliwaambia waandishi Jumamosi na kuongeza:
"Ninaweza kuamua iwapo nitaondoka au nitasalia lakini uamuzi wa mwisho ni wa klabu ya Chelsea - iwapo wanataka niondoke."
Hazard ambaye anatajwa kuwaniwa kwa ukaribu na Real Madrid, ameishauri Chelsea kufanya usajili wa maana kabla ya msimu kuanza.
Chelsea ilimpiga kalamu meneja wake Antonio Conte Ijumaa na kumnasa raia mwenzake wa Italia Maurizio Sarri, chini ya saa 24
Comments
Post a Comment