BAADA YA UFARANSA KUBEBA UBINGWA WA WORLD CUP, KOCHA WA MESSI AONDOLEWA KAZINI



Muda mfupi baada ya Ufaransa kuhitimisha michuano ya Kombe la Dunia kwa kutwaa ubingwa, upande wa pili Shirikisho la Soka la Argentina (AFA), wamekubaliana na Kocha Jorge Sampaoli kufikia tamati ya mkataba wao.
Sampaoli anaondoka Argentina baada ya kikosi chake kuboronga katika michuano ya Kombe la Dunia.
Imeelezwa pande zote mbili zimeelewana. Pia Kocha wa viungo na Kocha wa mafunzo ya video nao wameachia ngazi.
Sampaoli alikiongoza kikosi cha Argentina katika michuano hiyo mpaka hatua ya 16 bora na kutolewa nje na Ufaransa kwa kipigo cha mabao 4-3.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!