HABARI ZA KITAIFASALUM KIHIMBWA AONGEZA MKATABA MTIBWA SUGAR




KLABUya Mtibwa Sugar Sports Club imefanikiwa kuingia mkataba mpya na kiungo mshambuliaji wake Salum Ramadhani Kihimbwa.

Salum Kihimbwa alikuwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na sasa ameongeza miaka miwili hivyo Salum Ramadhani Kihimbwa mkataba wake na Mtibwa Sugar ni wa miaka mitatu na unatarajia kufikia tamati 2021.
Akizungumza leo mjini Dar es Salaam, Katibu Msaidizi  wa Mtibwa Sugar, Abubakar Swabur juu ya mkataba wa Kihimbwa amesema wameboresha mkataba wa awali na hivyo ataendelea kuitumikia Mtibwa kwa misimu mitatu zaidi na hii ilitokana na kiwango chake katika msimu wa kwanza
“Tumefikia makubaliano na Salum Kihimbwa ya kuongeza miaka miwili na alikuwa amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wa awali hivyo mkataba huu  ni wa miaka mitatu na utafikia kikomo 2021, ni furaha kwetu kwa kwakuwa tumemuongeza mkataba mtu sahihi kutokana na kipaji kikubwa alichonacho” Abubakar Swabur.
Salum Ramadhani Kihimbwa alijiunga na Mtibwa Sugar akitokea Polisi Morogoro inayocheza ligi daraja la kwanza msimu jana na pia amewahi kuitumikia Mkamba Rangers ya Kilosa Morogoro.
Kiungo huyo mshambuliaji pia ametoa mchango mkubwa kwa wana tam tam msimu 2017/2018  baada kuwa mmoja ya wachezaji waliobeba kombe la Azam Sports Federation Cup.
Mshindi wa tuzo mbili katika msimu 2017/2018, Salum Kihimbwa alishinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa Mtibwa Sugar na tuzo yake ya pili ilikuwa tuzo ya goli bora la msimu na goli lake lilikuwa dhidi ya Singida United katika fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!