Posts

CHIRWA ABAKI DAR KWENYE MECHI YAO NA SHELISHELI

Image
Kikosi cha Yanga kimeondoka asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam kwenda Shelishli kwa ajili ya mchezo wa marudiano hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Saint Louis Suns utakaofanyika Jumatano mjini humo. Safari hiyo imekuja huku mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akilazimika kubaki Dar kutokana na kuwa majeruhi.  Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema Chirwa pamoja na kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Donald Ngoma hawajasafiri kutokana na kutokuwa fiti kiafya. Wachezaji wengine majeruhi ambao nao hawajasafiri ni beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na mshambuliaji Mrundi Amissi Tambwe. Kikosi cha kamili cha Yanga kilichopondoka leo asubuhi ni: Makipa: Ramadhani Kabwili, Beno Kakolanya na Youthe Rostand. Mabeki: Hassan Kessy, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Gardiel Michael, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Patto Ngonyani na Kelvin Yondani. Viungo: Said Juma ‘Makapu’, Papy Kabamba Tshishimbi, Pius Buswita, Raphael Daud, Yussuf Mhilu, Ibrahim Ajib, Said Muss...

KIKOSI CHA SIMBA -DJIBOUT KWA AJILI YA MCHEZO WAO NA GENDARMERIE KESHOKUTWA JUMANNE

Image
Kikosi cha Simba kimeondoka jioni ya leo kwenda nchini Djibout kwa ajili ya mchezo wao wa pili dhidi ya Gendarmerie Nationale, keshokutwa Jumanne. Kikosi kilichosafiri leo kuelekea Djibout ni:-  (1) Aishi Salum Manula (2) Emanuel Elias Mseja (3) Mohamed Hussein Mohamed (4) Mzamiru Yassin Said (5) Bukaba Paul Bundala (6) Emmanuel Arnold Okwi (7) Moses Peter Kitandu (8)Shiza Ramadhani Yahya (9) Nicholas Gyan (10) Erasto Edward Nyoni (11) James Agyekum Kotei (12) Shomari Salum Kapombe (13) Mwinyi Kazimoto Mwitula (14) Jonas Gellard Mkude (15) John Raphael Bocco (16) Ally Shomary Sharifu (17) Said Hamisi Juma (18) Yusufu Seleman Mlipili (19) Murushid Juuko (20) Kwasi Asante

KAMA KAWA HAJI MANARA HAWEZI KUWAACHA YANGA HIVIHIVI

Image
Simba na Yanga zipo nje ya mipaka ya Tanzania kwa ajili ya michezo yao ya kimataifa iliyopo chini ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), lakini huku nyuma hawajaondoka hivihivi. Kama kawaida yake Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwafanyia utani wapinzani wao wa jadi, Yanga kutokana na kuondoka nchini wakiwa wamevaa kaptura huku mmoja wa wachezaji wa Yanga akionekana ameshusha kaptura yake kwa chini kwa staili maarufu ya ‘kata K’. Manara aliweka picha ambayo inawaonyesha wachezaji wa Yanga wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kisha akaandika ujumbe huu: “Tofauti ya jumlisha na Msalaba...Tofauti ya Tende na Mende, malizia na tofauti ya Jua na Mvua......kupanga ni kuchagua......”  Baada ya hapo akaandika: “Loooh hizi kata K zingine bana! Boxer nje nje...ila ndiyo ukimataifa huo au siyo! Swap uone tofauti yao na yetu...au sisi tunapendelewa hivi vifaa?🤔🙇” Aidha, Manara aliamua kuweka pi...

YANGA KUKWAMA KIMATAIFA,SIMBA KUPETA SHIRIKISHO

BOCCO NDIYE MSHAMBULIAJI BORA TANZANIA

Image
Simba imeendea kuwa na mwendelezo mzuri katika msimu huu wa 2017/18, ambapo inaongoza Ligi Kuu ya Vodacom na imeanza kwa kishindo katika Kombe la Shirikisho Afrika, lakini nyuma ya pazia kuna wachezaji ambao wamekuwa wakionyesha uwezo wa juu. Kuna wachezaji kadhaa wa timu hiyo ambao wameonyesha ni msaada wa Simba kwa safari hii, baadhi yao ni Emmanuel Okwi na Asante Kwasi, lakini kuna mtu anaitwa John Bocco huyu amekuwa akiwakosha mashabiki wengi wa Msimbazi kwa kasi yake ya kutupia. Mchambuzi wa masuala ya soka nchini Tanzania, Edo Kumwembe amemzungumzia mshambuliaji huyo wa Simba, John Bocco kwa kusema kuwa ndiye mshambuliaji bora kuliko wote kwa sasa nchini Tanzania kwa wazawa. Edo amesema hayo alipokuwa akichambua michezo leo asubuhi katika kituo cha Radio cha EFM ambapo alisema Bocco anastahili sifa hizo kwa kile ambacho amekuwa akikionyesha. “Ukiondoa kina Mbwana Samatta na Simon Msuva ambao wapo nje ya Tanzania, kwa sasa Bocco ndiye mchezaji bora kwa washambuliaji wa T...

MZEE MWINYI ATENGUA KAULI YA TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU

Image
Baada ya kupita miaka mingi, hatimaye, rais mstaafu wa awamu ya pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi ametengua kauli yake juu ya soka la Tanzania. Mzee Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika (Caf), kati ya Simba dhidi ya Gendarmerie ulioshuhudiwa Simba ikipata ushindi wa mabao 4-0. Mzee Mwinyi alivutiwa na soka la Simba lililoonyeshwa kwenye mchezo huo na baada ya mechi alifuta kauli yake aliyoitoa miaka 30 iliyopita aliposema “Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu” . Akizungumza baada ya mchezo huo wa jana uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Mzee Mwinyi alisema:  “Nimeshuhudia mchezo mzuri na sasa nafuta lile neno kwamba Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kila anaetaka kujifunza kunyoa atunyoe sisi, sasa nyie ndio vinyozi.”

WALICHOKISEMA AZAM KUHUSU OKWI NA JONAS MKUDE