Posts

HIZI NDIYO REKODI ZA TANZANIA PRISONS VS AZAM FC

Image
Kuelekea mchezo wa Tanzania Prisons dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Sokoine kuna mambo kadhaa yanahohusu mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom utakaopigwa leo Jumapili. Rekodi zinaonyesha kuwa hadi sasa, kihistoria timu hizo zimekutana mara 14 kwenye mechi za ligi, Azam FC ikiwa na rekodi ya kushinda mara tano, Prisons yenyewe mara tatu ikiibuka kidedea huku ikishuhudiwa mechi sita zikiisha kwa sare. Azam FC ambayo inauchukulia kwa uzito mkubwa mchezo huo hasa ikitaka kuifikia Simba kwenye mbio za ubingwa, ilipata ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa mwisho uliofanyika uwanjani hapo msimu uliopita. Bao pekee la Azam FC lilifungwa kiustadi kwa shuti na aliyekuwa kiungo mkabaji wa timu hiyo, Michael Bolou, bao lililofanya rekodi kuandikwa upya kwa mabingwa hao kupata ushindi wa kwanza Sokoine dhidi ya Prisons kwenye mechi saba walizocheza ndani ya dimba hilo. Ukiondoa mechi moja ambayo Azam FC imeitambia Prisons, mechi nyingine sita zilizobakia zilizopigwa mjini Mbeya, maafan...

RUVU SHOOTING 0-1 YANGA ‘LIVE’ FULL TIME, UWANJA WA TAIFA Harun Habari Za Kitaifa 21 January 2018 FacebookTwitter

Image
FULL TIME Dakika ya 95: Mchezo umemalizika, Yanga inapata ushindi wa bao 1-0, mfungaji ni Buswita. Dakika ya 94: Yanga bado wanamiliki mpira muda mwingi. Dakika ya 90: Zinaonyeshwa dakika tano za nyongeza. Dakika ya 88: Juma Mahadhi anakosa nafasi ya wazi, akiwa yeye na lango anashindwa kuugusa mpira ujae wavuni. Dakika ya 82: 84: Kasi ya mchezo imepungua kiasi. Dakika ya 81: Ruvu wanamtoa Abdul Mussa anaingia Khamis Mcha. Dakika ya 76: Issa Kanduru anapata kadi ya njano kw akumchezea faulo Hassan Kessy. Dakika ya 71: Dante yuko chini baada ya kusukumwa na Kanduru. Dakika ya 70: Pius Buswita anapewa kadi ya njano baada ya kuchomekea mguu Rajab Zahiri. Dakika ya 68: Tambwe anatoka, nafasi yake inachukuliwa na Juma Mahadhi. Dakika ya 67: Mwamuzi anatoa kadi kwa Damas Mwakwaya baada ya kumsukuma Ajibu na mashabiki Yanga kulalamika. Fakika ya 66: Ajibu anapata kadi ya njano kwa kumsukuma beki wa Shooting. Dakika ya 65: Issa Kanduru anakosa nafasi ya wazi akiwa ...

OKWI HUYU HAPA:ATUMA SALAMU MECHI IJAYO YA KAGERA SUGAR

Image
MSHAMBULIAJI Mganda Emmanuel Arnord Okwi ametokea benchi na kufunga mabao mawili Simba SC ikishinda 4-0 dhidi ya Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Matokeo hayo yanaifanya Simba SC ifikishe pointi 29, baada ya kucheza mechi 13, ikiwazidi pointi saba mabingwa watetezi, Yanga SC na pointi mbili Azam FC wenye 27 katika nafasi ya pili, wakati Mtibwa Sugar sasa ni ya tatu kwa pointi zae 24 baada ya timu zote kucheza mechi 13.Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Jacob Adongo wa Mara, aliyesaidiwa na Mohammed Mkono wa Tanga na Gasper Ketto wa Arusha hadi mapumziko Simba SC walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-0.Kiungo Shiza Ramadhani Kichuya alianza kuifungia Simba SC dakika ya tatu akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo mkongwe Mwinyi Kazimoto, kufuatia John Raphael Bocco kuangushwa nje kidogo ya boksi. Singida wakacharuka na kuanza kupeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa Simba kusaka bao la kusawazisha, ...

YALIYOANDIKWA KATIKA MAGAZETI YA MICHEZO LEO JUMAMOSI, TAREHE 20.01.2018

Image

MECHI YA SIMBA VS SINGIDA UNITED IMEMPA NDEMLA GARI

Image
Mwenyekiti wa Kamtai ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ametoa zawadi ya gari kwa mchezaji wa Simba, Said Hamis Ndemla. Hans Poppe ametangza kumpa Ndemla gari baada ya kuonyesha kiwango kizuri cha kuvutia katika mechi dhidi ya Singida United, jana. Simba imeshinda kwa mabao 4-0 katika mechi hiyo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini. Ndemla alitengeneza mabao mawili moja akifunga Emmanuel Okwi na jingine Asante Kwasi. Hans Poppe amesema mechi ya leo imekuwa ni fainali ya uamuzi wake lakini amekuwa akimfuatilia Ndemla. “Nilikuwa nikimfuatilia kama ambavyo nimekuwa nikisema nahitaji mchezaji mwenye nidhamu na ambaye hawezi kubadilika. Utaona Ndemla amekuwa benchi lakini akiingia uwanjani anaonyesha mchango wake,” alisema. “Tena pamoja na kukaa benchi, hakuwahi kuonyesha utovu wa nidhamu. Badala yake kila akipata nafasi amekuwa akijituma na kuisaidia timu.” Hii ni mara ya pili Hans Poppe anatoa gari kwa mchezaji wa Simba. Alianza na Hussein Z...

SIMBA YAMTAMBULISHA RASMI 'MFARANSA' PIERRE LECHANTRE

Image
Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, hii leo Ijumaa imemtambulisha rasmi kocha mkuu mpya wa timu hiyo, Pierre Lechantre amabye amechukua nafasi iliyoanchwa na Joseph Omog aliyetimuliwa hivi karibuni. Kocha Pierre Lechantre ametambulishwa katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena jijini Dar tukio lililoendana na kusainishana mikataba. Kocha huyo ametua nchini Tanzania akiwa pamoja na kocha wa viungo Amin Mohamed Habib ambapo kwa pamoja watafanya kazi na Masoud Djuma ambaye ndiyo yupo kikosini kwa sasa. Kocha Lechantre amewahi fundisha timu ya taifa ya Cameroon iliyochukua ubingwa wa Afrika. Kikosi cha Simba chenyewe kipo mjini Bukoba kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Jumatatu ijayo, hivyo, Lechantre ataanza kazi mara moja timu itakaporejea Jumanne baada ya mchezo huo.  Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara pia amewashukuru mashabiki wa Simba kwa sapoti ambayo wameionyesha wakati mchakato ulipokuwa ukiendelea. Hii ni mara ya kwanza kwa kocha...

MFUMO WA 3-5-2 NDIYO SILAHA YENYE SUMU KALI KWA SIMBA

Image
Ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Singida United umempa nafasi ya kuzungumza Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi Masoud Juma ambaye amesema kuwa wachezaji wameanza kuuzoea mfumo wake mpya na kuwazodoa waliokuwa wakimpinga awali. Akiiongoza Simba katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya Joseph Omog kuondolewa, Djuma alishindwa kuifanya Simba kutamba na matokeo yake ikaonekana kuwa ni timu ya kawaida. Kutofanya vizuri katika michuano ya Kombe la Mapinduzi kukasababisha baadhi ya mashabiki na wadau wa timu hiyo kuona kocha huyo hafai, lakini kiwango kizuri dhidi ya Singida United, Alhamisi iliyopita kimerejesha imani ya Wanasimba wengi kwa kocha huyo msaidizi. Mara baada ya mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ea Salaam, Djuma alisema mfumo wa 3-5-2 unahitaji wachezaji kujituma zaidi na wanapofika kwenye eneo la 18 la wapinzani wanatakiwa kushambulia sana, lakini wachezaji walikuwa hawajazoea kwa kuwa lilikuwa suala jipya kwao.  Amesema mchezo huo haikuwa r...