Zahera afumua kikosi chote Yanga
Kikosi cha yanga kilichofungwa na Polisi Tanzania KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera ameamua kufumua kikosi chote huku akisisitiza kwamba hafanyi mambo kufurahisha mashabiki. Zahera amekwenda mbali na kusisitiza kwamba hata katika mechi ya kirafiki leo Jumapili dhidi ya AFC Leopards hakuna hata mchezaji mmoja aliyecheza Moshi dhidi ya Polisi Tanzania atakayeanza. Katika mechi dhidi ya Polisi juzi Ijumaa Yanga ilifungwa mabao 2-0 huku ikianzisha sura nyingi mpya. Zahera amekwenda mbali zaidi kwa kusema kwamba hata kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Township Rollers hakuna mchezaji yoyote aliyecheza dhidi ya Polisi ataanza. Kikosi cha kwanza kilichoanza dhidi ya Polisi kilikuwa na Ramadhani Kabwili,Mustafa Seleman,Gustava Saimon,Ally Ally,Kelvin Yondani,Abdulaziz Makame,Maybin Kalengo,Feisal Salum,David Molinga na Deus Kaseke. Kocha huyo anayezungumzia Kiswahili cha lafudhi ya Kicongo amesisitiza kwamba anakifanyia mabadiliko makubwa kikosi hicho ili kupata ubora ana...