Posts

Showing posts from March, 2019

YANGA WATINGA NUSU FAINALI FA, YAIPIGA ALLIANCE KIRUMBA

Image
KLAUS Kindoki leo amekuwa shujaa wa Yanga baada ya kuokoa penalti ya mwisho iliyopigwa na nahodha wa timu ya Alliance FC, Siraj Juma. Dakika 90 za mchezo wa leo wa hatua ya fainali ulikamilika kwa Alliance kutoshana nguvu na Yanga kwa kufungana bao 1-1. Yanga walitangulia kufunga bao dakika ya 38 lililofungwa na Heritier Makambo na kwa upande wa Alliance bao lilifungwa na Johson James. Klaus Kindoki Baada ya mwamuzi kuamua matuta, Yanga walianza kupiga kupitia beki kisiki Kelvin Yondani ambaye aligongesha kwenye mwamba, Paul Godfery alifunga penalti yake,Thaban Kamusoko alifunga kwa staili ya paneka, Mrisho Ngassa penalti yake iligonga mwamba na Haruna Moshi alifunga penalti kiufundi. Kwa upande wa Alliance penalti ya kwanza ilifungwa na Joseph John, Martin Kigi aligongesha kwenye mwamba, Dickson Ambundo alikosa penalti yake, Jofrey Luseke na Samir Vicent alifunga penalti. Baada ya kumaliza penalti 5 za awali kwa timu zote matokeo yalisoma 3-3 baada ya Yanga ku...

REAL MADRID YAMTENGEA POGBA BILIONI 381

Image
Staa wa Manchester United, Paul Pogba REAL Madrid inataka kuanza mikakati rasmi ya kumsajili staa wa Manchester United, Paul Pogba mwishoni mwa msimu huu. Hatua hiyo imefikiwa baada ya Pogba mwenyewe ambaye ana umri wa miaka 26 kufunguka kuwa ana ndoto ya kuichezea timu hiyo siku moja. Pogba alikiri hivyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwa katika majukumu ya kuichezea timu yake taifa ya Ufaransa, kauli hiyo imedaiwa kuiamsha Madrid katika mpango wa kukamilisha dili. Pogba alieleza kuwa anatakani siku moja afanye kazi na Zinedine Zidane ambaye ni kocha wa sasa wa Madrid. Imefahamika kuwa Real Madrid imetenga pauni milioni 125 (Sh bilioni 381) kwa ajili ya kumsajili kiungo huyo. Ikumbukwe kuwa Pogba aliitosa Real Madrid na kuamua kusajiliwa na Manchester United kwa pauni milioni 89, miaka miwili iliyopita. Madrid wanajua kuwa Mfaransa huyo ana furaha kwenye timu yake ya sasa lakini hana mpango wa kumalizia maisha yake ya soka akiwa klabuni ha...

ZAHERA: MSITETEMEKE WAACHENI WAENDE, TIMU ITAKAA VIZURI – VIDEO

Image
WAKATI Timu ya Yanga ikitarajiwa kutua uwanjani leo Jumamosi, Machi 30, 2019 kukipiga na Alliance FC, mchezo wa hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho la Azam katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza, kocha mkuu wa Yanga, Raia wa DRC, Mwinyi Zahera amesema kuwa hana hofu na mchezo huo licha ya kukosekana kwa nyota wake wa kikosi cha kwanza akiwemo Ibrahim Ajibu. Akizungumzia kuhusu mchezo huo huku timu yake ikiwakosa wacheza sita wa kikosi cha kwanza, Zahera amesema; “Juma Abdul, Mohamed Banka, Haji Mwinyi, Ibrahim Ajibu hawa wamebaki Dar, Gadiel Michael yeye amekwenda Afrika kusini kwa ajili ya majaribio, Ramadhan Kabwili yupo kwnye Timu ya Taifa chini ya miaka 20. “Sina mashaka, nipo tayari kwa mchezo wangu wa kesho na nimewaambia wachezaji wangu wapambane na tutapata matokeo kila kitu kinawezekana, kama mchezaji anataka kuondoka kwenye klabu akatafute maisha kwingine, mwacheni ande wala msitetemeke, Yanga ni timu kubwa na itakaa vizuri tu” amesema Zahera. VIDEO:...

YANGA SC: TULIENI, TUNAWAPIGA ALLIANCE KWAO

Image
BEKI kitasa mkongwe wa Yanga, Kelvin Yondani amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo watakapowavaa wapinzani wao Alliance FC, katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho (FA). Timu hizo zinatarajiwa kuvaana leo kwenye Uwanja  wa CCM Kirumba mkoani Mwanza, mchezo unaotarajiwa kujaa upinzani mkubwa. Huo ni mchezo wa pili timu hizo kukutana kwenye uwanja huo na mechi yao ya kwanza kucheza ilikuwa ya Ligi Kuu Bara ambayo ilimalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0 lililofungwa na Mrundi, Amissi Tambwe aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Deus Kaseke. Akizungumza na Championi Jumamosi, Yondani alisema anafahamu ubora wa kikosi cha Alliance, lakini hana hofu ya kupata ushindi katika mchezo huo. Yondani alisema, katika msimu huu wamepanga kuchukua mataji yote wanayoyashindania ubingwa ukiwemo wa ligi na Kombe la Shirikisho linaloshikiliwa na Mtibwa Sugar ambao wameondolewa tayari katika mashindano hayo. “Tumeanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Alliance muda mrefu na hiyo ...

SOLSKJAER SASA NATAKA UBINGWA PREMIER

Image
KOCHA Ole Gunnar Solskjaer ameahidi kupambana kwa ajili ya kurejesha sifa ya timu yake ya Manchester United katika kupigania mataji. Kocha huyo ambaye klabu yake inamiliki Uwanja wa Old Trafford alitangazwa kuwa kocha rasmi wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kuwa wa muda kwa miezi mitatu, ameahidi kuwa hilo la ubingwa ndilo ambalo analifikiria. Mkataba wake ni wa pauni milioni 7 kwa mwaka, ukiwa umechagizwa na kurejesha ushindi kikosini hapo baada ya kuwa na msimu mbovu chini ya Kocha Jose Mourinho ambaye alifukuzwa Desemba, mwaka jana. “Ubingwa wa Premier League ndilo tunalowaza kwa sasa, kunyanyua taji ndilo jambo muhimu kwetu, tunataka kurejesha hali hiyo japokuwa siyo kazi nyepesi. “Nataka nikiondoka niwe nimeshinda mataji, likiwemo la Premier League, ikiwa hivyo nitakuwa najivunia uwepo wangu klabuni hapa,” alisema Ole na kuongeza: “Nina furaha na ni mtu ninayepambana, nataka siku nikiondoka niwe na heshima.” Wakati huohuo, United imeamua kuto...

ZAHERA AWATEMA AJIBU, YONDANI YANGA SC

Image
Ibrahim Ajibu (kushoto) akifanya yake. KOCHA Mkuu wa Yanga, Mkongoni, Mwinyi Zahera ameamua kuvunja ukimya baada ya kusema mchezaji yeyote ambaye anataka kuondoka ndani ya kikosi hicho ni ruksa. Kwa sasa kumekuwa na tetesi za mastaa kibao wa timu hiyo wakihusishwa na timu nyingine kama Ibrahim Ajibu, Kelvin Yondani na Papy Kabamba Tshishimbi ambao wanaripotiwa kutakiwa na Simba. Kutokana na tetesi hizo, Kocha Zahera alisema kuwa, haogopi kusikia mchezaji fulani anaondoka kwenye kikosi chake kwa sababu kuna wakati wachezaji hao ambao wanatajwa kuondoka wanakuwa hawapo kwenye timu na bado wamekuwa wakipata matokeo. Kocha huyo alisema amekuwa akipigiwa simu na mashabiki ambao wamekuwa wakihoji kuwa wamekuwa wakisikia wachezaji Tshishimbi, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Yondani lakini yeye amekuwa akiwaambia wasijali mambo yatakwenda sawa hata kama wataondoka. Zahera aliongeza kuwa tayari ameshawaambia viongozi wa timu hiyo kuwa hawapaswi kutetemeka wala kuwa na hofu...

SIMBA WASINGIZIA JAMHURI MOROGORO

Image
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, anakuna kichwa juu ya mbinu gani atumie wakati kikosi hicho kikiwa kinacheza katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro baada ya kusema wazi uwanja huo ni mbovu na hauendani na staili wanayocheza. Simba wamelazimika kuhamia huko baada ya Uwanja wa Taifa waliokuwa wanautumia kupigwa kufuli kwa ajili ya matengenezo kabla ya Afcon ya vijana. “Ndiyo tunaweza kuathirika kwa namna fulani kwa sababu pale Taifa sehemu ya kuchezea ni safi tofauti na Morogoro ambapo tunaenda kucheza kwa sasa. “Tunahama kutoka sehemu nzuri na kwenda pasipo pazuri. Pale sehemu yake ya kuchezea wala siyo rafiki sana, kucheza pale inabidi tujiandae sana bila ya hivyo inaweza kutukwamisha na kushindwa kupata ushindi,” alimaliza kocha huyo aliyejenga imani kwa mashabiki wa Simba.

MAN U YAMPA SOLSKJAER MKATABA WA KUDUMU

Image
Ole Gunnar Solskjaer HATIMAYE klabu ya  Manchester United imemchukua rasmi Ole Gunnar Solskjaer kuwa kocha na kumpa mkataba wa miaka mitatu baada ya kung’ara katika kipindi alichofanya kazi kama kocha wa muda. Kocha huyo raia wa Norway alifufua nguvu za klabu hiyo tangu akabidhiwe timu baada ya kutimuliwa kwa Mreno Jose Mourinho mwezi Desemba mwaka jana.  Tangu hapo ameshinda mechi 14 kati ya 19 na kuwaongoza Mashetani Wekundu hao kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya. Solskjaer, ambaye alifunga mabao 126 katika mechi 366 alizoichezea United, na alishakuwa shujaa kwa mashabiki wa klabu hiyo ya soka, alijipatia sifa ya kuwa mtu aliyefunga bao katika muda wa majeruhi wa fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mwaka 1999 na kuiwezesha timu hiyo kutwaa vikombe vitatu katika msimu mmoja. “Kutoka siku ya kwanza niliyowasili, nilijisikia kama niko nyumbani katika klabu hii ya aina yake,” Solskjaer alisema katika taarifa yake iliyowekwa kwenye tovuti ya kla...

ZAHERA AWAPA YANGA MIL.60, NYIKA AJIUZULU

Image
Kocha Mwinyi Zahera AMSHAAMSHA ya Kocha Mwinyi Zahera ikichagizwa na Kamati ya Uhamasishaji ya Yanga, imekusanya shilingi 60,089,047. Zahera ndiye aliyeanzisha zoezi hilo la uchangishaji wa fedha zitakazotumika kwa ajili ya kusajili wachezaji watakaowatumia msimu ujao. Mratibu wa timu hiyo, Hafi dh Saleh alisema fedha hizo wamezikusanya kupitia akaunti mbalimbali ikiwemo ya CRDB Benki ni Shilingi 54,594,079, M-Pesa 2,530,550 na TigoPesa ni 2,964, 418 pekee. Mratibu huyo amewataka mashabiki wa timu hiyo kuongeza kasi ya kuichangia timu yao ili kufanikisha malengo ya kufi kia shilingi bilioni 1.5 anazozihitaji kocha kwa ajili ya usajili katika msimu ujao. Katika hatua nyingine, Kaimu Mwenyekiti na Mjumbe wa Yanga, Samuel Luckumay na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano, Hussein Nyika, wamejiuzulu katika nafasi zao. Luckumay alisema kuwa: “Lengo ni kupisha Uchaguzi Mkuu wa Yanga na kikubwa tumeona siyo vema kufanya uchaguzi mkuu wa nchi na klabu, mwakani katika k...

SPOTI HAUSI: UKWELI KUHUSU USAJILI WA ‘TUYISENGE’ SIMBA – VIDEO

Image
March 28, 2019  Kipindi cha Spoti Hausi leo kipo tena hewani ambapo wachambuzi wako watakuwa wakikuletea uchambuzi mbalimbali kuhusu kufuzu kwa Stars kwenye Kombe la Mataifa Afrika, maandalizi ya Simba ya mechi ya Simba na TP Mazembe. Lakini pia kuna ukweli gani juu ya mshambuliaji wa Gor Mahia, Tuyisenge ambaye anatajwa kuwa hapa nchini kwa ajili ya kujiunga na Simba.

ZAHERA AONDOKA NA NYOTA 20 KWENDA MWANZA

Image
Kikosi cha timu ya Yanga. KOCHA Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera jana usiku alitarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam akitokea nyumbani kwao DR Congo kabla ya kesho Alhamisi kukwea pipa kwenda mkoani Mwanza na nyota wake 20. Kocha huyo alikuwepo nyumbani kwao DR Congo akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya nchi hiyo anakofundisha kama kocha msaidizi ilipokuwa ikicheza na Liberia katika fainali za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika na kufanikiwa kufuzu. Mkongomani huyo, aliukosa mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara walipocheza na Lipuli FC ambao walifungwa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Haruna Shamte. Akizungumza na  Championi Jumatano , mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema kuwa kocha huyo alitarajiwa kurejea Dar jana kwa ajili ya mchezo huo wa Kombe la Shirikisho. Saleh alisema, kocha huyo alizuia timu hiyo isisafiri hadi yeye atakaporejea nchini kwa ajili ya kujiunga na kikosi hicho kilichopania kuchukua Kombe hilo la Shirikisho msimu huu. Alio...

KOTEI ABADILI URAIA, SASA ANAITWA JAMES MAGUFULI

Image
KATIKA kile ambacho kilionekana kuongeza hamasa kwa  Watanzania  kuelekea katika mchezo wa timu ya taifa hilo,  Taifa Stars  dhidi ya  Uganda ‘The Cranes’ , kiungo wa  Simba, James Kotei  alitangaza kujibadili uraia kwa muda. Kotei ambaye ni raia wa  Ghana , aliamua kutangaza kuwa ataiunga mkono  Stars  kisha moja kwa moja akasema yeye ni Mtanzania kwa muda na akajipa jina kabisa kuwa anaitwa  James Magufuli. Stars ilikuwa uwanjani jana kuivaa  Uganda  katika mchezo wa  Kundi L  kuwania kufuzu fainali za  Mataifa ya Afrika  ( Afcon 2019 ), ushindi pekee ulikuwa na nafasi kubwa ya kuifanya Tanzania ifuzu kucheza michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu ilipofanya hiyo mwaka 1980. Akitumia ukurasa wake wa  Twitter, Kotei  aliweka picha kadhaa akiwa amevaa jezi ya Taifa Stars pamoja na baadhi ya mashabiki wengine wa soka ambao nao walikuwa wamevaa jezi hizo. “Samahani sana...

MWAKINYO ATEMBELEA GLOBAL, ATAMBA HAJAONA WA KUPIGANA NAYE NCHINI

Image
Bondia Hassan Mwakinyo (kulia) akisalimiana na Meneja wa Global Group Abdallah Mrisho ofisini, Sinza Mori, Dar BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo, amesema kuwa hajaona bondia wa kupigana naye hapa nchini na jeuri hiyo anaipata kutokana na udhamini anaoupata kutoka Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Michezo, SportPesa. Bondia Hassan Mwakinyo (Kulia) akisalimiana na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally, leo Ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori, Dar. Kauli hiyo, aliitoa leo Jumanne mara baada ya kutembelea ofisi za Global Group inayochapisha magazeti ya  Championi, Spoti Xtra, Uwazi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi Mchanganyiko, pamoja na vituo vya mtandaoni vya Global TV Online na +255 Global Radio,  Sinza-Mori jijini Dar es Salaam. Bondia Hassan Mwakinyo akifafanua jambo kitaalamu kwa Mhariri Mtendaji wa Global Group Saleh Ally. Mwakinyo, wikiendi iliyopita alifanikiwa kumpiga mpinzani wake Muargentina, Sergio Gonzalez ...