HABARI ZA KITAIFASALUM KIHIMBWA AONGEZA MKATABA MTIBWA SUGAR
KLABUya Mtibwa Sugar Sports Club imefanikiwa kuingia mkataba mpya na kiungo mshambuliaji wake Salum Ramadhani Kihimbwa. Salum Kihimbwa alikuwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na sasa ameongeza miaka miwili hivyo Salum Ramadhani Kihimbwa mkataba wake na Mtibwa Sugar ni wa miaka mitatu na unatarajia kufikia tamati 2021. Akizungumza leo mjini Dar es Salaam, Katibu Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Abubakar Swabur juu ya mkataba wa Kihimbwa amesema wameboresha mkataba wa awali na hivyo ataendelea kuitumikia Mtibwa kwa misimu mitatu zaidi na hii ilitokana na kiwango chake katika msimu wa kwanza “Tumefikia makubaliano na Salum Kihimbwa ya kuongeza miaka miwili na alikuwa amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wa awali hivyo mkataba huu ni wa miaka mitatu na utafikia kikomo 2021, ni furaha kwetu kwa kwakuwa tumemuongeza mkataba mtu sahihi kutokana na kipaji kikubwa alichonacho” Abubakar Swabur. Salum Ramadhani Kihimbwa alijiunga na Mtibwa Sugar akitokea Polisi Morogoro ...