Posts

Showing posts from February, 2019

AZAM WAPOKEA CV 10 ZA MAKOCHA KWA SIKU MOJA

Image
MARA baada ya  Azam  kumvunjia mkataba kocha wake  Mholanzi, Hans van Der Pluijm  mapema juzi, imebainika kwamba uongozi huo tayari umepokea zaidi ya wasifu wa makocha 10 ambao wameomba kibarua kikosini hapo. Azam FC, juzi Jumamosi walitangaza kuachana na Pluijm pamoja na msaidizi wake, Juma Mwambusi ikiwa ni baada ya timu hiyo inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu, kuwa na matokeo mabaya kwenye mechi zake tano zilizopita ikiwemo ya Simba. Lakini ndani ya siku moja tu, tayari wameshapokea wasifu ‘CV’ za makocha 10. Makamu Mwenyekiti wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, amesema mara baada ya wao kuachana na Pluijm, tayari hadi jana walikuwa wamepokea ‘CV’ za makocha wapatao 10 ambao wanataka mikoba ya Mholanzi huyo ingawa kwa sasa timu ipo chini ya makocha wa muda, Meja Abdul Mingange na Idd Cheche kutoka timu za vijana za Azam.  “Idadi inaongezeka tu kila mara lakini tukishakaa viongozi ndiyo tutaamua tufanye nini,”  alisema Popat. ...

KAGERE, BOCCO WAMPA JEURI MBELGIJI KWA WAARABU

Image
K ASI  ya safu ya ushambuliaji ya Simba, imempa jeuri Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Patrick Aussems akitamka kuwa ana matumaini makubwa ya kuwafunga wapinzani wao JS Saoura nchini kwao Algeria. Simba inatarajiwa kuvaana na Saoura Machi 9, mwaka huu huko Algeria katika mchezo wa marudiano baada ya mchezo wa awali kushinda mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Safu ya ushambuliaji ya Simba inaongozwa na Mnyarwanda, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na John Bocco ambayo imefanikisha ushindi wa michezo minne migumu mfululizo dhidi ya Al Ahly 1-0, Yanga 1-0, African Lyon 3-0 na Azam FC 3-0. Akizungumza na  Championi Jumatatu,  Aussems alisema kuwa anafurahishwa na kasi hiyo ya ushambuliaji ambayo imeipa matokeo mazuri kutokana na kutimiza majukumu yao. Aussems alisema, bado anaendelea kuifanyia kazi safu hiyo ya ushambuliaji ili kuhakikisha wanaendelea na kasi hiyo ya kufunga kwenye michezo ijayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika watakapokutana na Saour...

MATOLA: TULIENI NIWAONYESHE NAMNA SIMBA INAVYOFUNGWA

Image
L ICHA  ya Simba kushinda mechi zake zote za hivi karibuni kwa kuanza na Mwandui 3-0, akafuata Mwarabu 1-0, African Lyon 3-0, Yanga 1-0 na Azam FC 3-1, kocha wa Lipuli, Selemani Matola amesema atawafunga Simba. Simba itacheza kesho na Lipuli mchezo wa ligi ikiwa ni kiporo kwenye Uwanja wa Samora huku rekodi zikionyesha kwamba tangu msimu wa 2017/2018 Lipuli ilipopanda daraja, hakuna hata timu iliyoonja ushindi kwa mwenzake. Akizungumza na  Championi Jumatatu,  Matola alisema amewatazama wapinzani wake kwa ukaribu na kujua udhaifu wao, hali ambayo imemfanya aamini kwamba kesho atavunja rekodi iliyowekwa kwa timu hizi mbili. “Siyo mechi rahisi, tumejipanga kamiligado, mechi tatu zimepita hakuna aliyebeba pointi tatu kwa mwenzie, sasa sisi tuna hamu sana kuwa wa kwanza kubeba pointi tatu nyumbani. “Najua Simba ni timu nzuri na ina kitu cha kipekee kwa sasa kutokana na ushindi ambao wamepata hivi karibuni, lakini hilo halitupi taabu kwa kuwa bado ni Simba wa...