BAADA YA KUFUZU KIBABE KWENDA 8 BORA CAF….HILI HAPA NENO LA MO DEWJI KWA SIMBA…

WAKATI Klabu ya Simba ikitangaza kuwa baada ya kumaliza mchezo wake dhidi ya CS Constantine, hesabu zote sasa zipo kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Tabora United, Mwekezaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohamed Dewji, amewapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kujituma uwanjani kiasi cha kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho. Akitoa salamu za pongeza jana, Dewji, ambaye ni Rais wa Heshima wa klabu hiyo, alisema kikosi cha timu hiyo kinaundwa na wachezaji wengi vijana wadogo, ambao ni wapya kwenye timu, wasio na uzoefu kwenye michezo mingi ya kimataifa, lakini wamekuwa wakijituma kweli kweli uwanjani na kuipatia ushindi, wakati mwingine ukiwa ni wa kushangaza kwenye dakika za majeruhi. “Niwapongeze wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, wanachama na mashabiki wa Simba kwa mshikamano na mafanikio makubwa yaliyopatikana tunayoshuhudia. Mafanikio haya si kazi ya mtu mmoja ni juhudi za familia mzima ya Wanasimba wote, pamoja na serikali yetu. “Kufu...